MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Sep 5, 2014

Mchekeshaji na mtangazaji wa kipindi cha ‘Fashion Police’ Joan Rivers afariki dunia

       joan_rivers Mchekeshaji maarufu na mtangazaji wa kipindi cha ‘Fashion Police’ nchini Marekani, Joan Rivers amefariki dunia, binti yake amesema. Rivers, 81, alikuwa amewekwa kwenye mashine ya kumsaidia kuishi katika hospitali ya Mount Sinai alikolazwa kwa shambulio la
moyo. Kwenye maelezo yake, binti yake, Melissa amedai kuwa mama yake amefariki akiwa amezungukwa na familia na marafiki na ameishukuru hospitali kwa uangalizi mzuri.
Melissa ni mtoto pekee wa Joan.
Ndoa yake ya kwanza ilidumu kwa miezi sita tu na ya pili na Edgar Rosenberg ilidumu kwa miongo miwili kabla ya mumewe kujiua mwaka 1987.