Akiongea na WAMBURABABU BLOG , Azma amesema ameamua kuachia wimbo wake huo
uitwao ‘Jinsi ya Kumkifikisha Mpenzi Wako Kileleni’, baada ya kuona
amekuwa akifanya nyimbo zenye ujumbe wa kijamii kwa muda mrefu lakini
watu wanazichukulia poa.
“Kikubwa nimeona nimefanya kazi nyingi sana zenye ujumbe mkubwa mfano
‘Mungu Inusuru Tanzania’, ‘Utata wa Katiba’, ‘Wanasubiri Nife’, ‘Kuwa
na Azma’, ‘Kila Kitu Kila Siku’, ambayo nimerelease last week lakini ndo
mapokeo yake ni madogo. Ndio maana nimeona nifanye kitu kingine ambacho
kiko negative ili nipime fikira za Watanzania pengine wanaweza kuvalue
kazi kubwa ninayofanya,” amesema Azma