"Yaani sijui hata nianzie wapi kuzungumzia hili la kutaka kufunga ndoa
na Diamond, naomba niseme ukweli kwamba nashangaa, kwanza sijui
chochote, nimekuwa nikiandikwa mara kwa mara lakini taarifa hizo wala
hazina ukweli wowote
.
.
“Mimi na Diamond ni tofauti kabisa, sijawahi kuwa na ukaribu naye.
Kwanza naumia sana na kutokwa na machozi kuendelea kusikia taarifa hizi
kuwa naolewa naye kitu ambacho hakipo kabisa, hata yeye mwenyewe
akisikia hivi anaweza kumtafuta mtu ambaye anasemwa kuwa anatoka naye
jambo ambalo si la kweli.”
“Wema namheshimu kama dada yangu, mtu ninayemjua kwenye tasnia ya filamu
Bongo, kwanza wote tunafanya sanaa japokuwa kwa upande wake anafanya
filamu na mimi muziki. Hizo taarifa juu ya kuniwinda sijui na
sijazisikia. Kiukweli zimenishtua sana.” Meninah
Diamond alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo hakupatikana kwa kuwa alikuwa ziarani barani Ulaya.