Mkurugenzi
Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mikazi Bw. Justo
Lyamuya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taratibu za upimaji wa
viwanja nchini na kutoa tahadhari kwa wananchi kutumia makampuni ambayo
hayakusajiliwa katika shughuli za upimaji Ardhi, wakati wa mkutano uliofanyika
leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu wa Baraza la Upimaji na Uthamini wa
Wizara Hiyo Bw. Nassor Duduma.
Katibu
wa Baraza la Upimaji na Uthamini wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Mikazi Bw. Nassor Duduma akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu ufuataji wa
Sheria katika shughuli za upimaji ardhi kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1957 sura
namba 324, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni
Afisa Habari wa Wizara Hiyo Bw. Clarence Nanyaro. Hassan
Silayo-MAELEZO
na JIACHIE BLOG / WAMBURABABU BLOG