Mgeni
rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere
(kushoto) akifuatilia maonyesho mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa
uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana, katikati ni Mtendaji mkuu TaSUBa Bw. Michael
J. Kadinde na kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
Mgeni
rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere
kati akipiga ngoma kama ishara ya uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa
lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
Mgeni
rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere
kulia akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TaSUBa Bw.
Ghonche Materego wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika
katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana. Picha hii
imechorwa sura ya Mhe. Makongoro na msanii aliyefaamika kwa jina la Sunday
Richard Kamangu.
Mgeni rasmi ambaye pia
ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kushoto akimpa
mkono wa pongezi msanii Sunday Richard Kamangu baada ya kupokea zawadi ya picha
iliyochorwa na msanii huyo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika
katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kushoto, na Mkurugenzi Msaidizi Sanaa
Bibi. Leah Kihimbi kulia wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yanaendelea
wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
Wasanii
kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa
lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.