Engineer
Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na
wanahabari kuhusiana na Tamasha la Upendo kwa mama ambalo linalenga
kutoa mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwawezesha
kujiajiri pamoja na kuwaombea na kuwashukuru kwa moyo wa upendo
waliyonayo kwa kujitoa katika kusimamia familia na malezi
Mratibu wa Tamasha la Upendo kwa mama Bw. Linus Kilembu akiongelea maandalizi ya Tamasha kuwa limekamilika kwa asilimia 90
Engineer
Carlos Mkindi mwenyekiti wa Tamasha la upendo ambaye ni mkurugenzi wa
mkundi production akifanyiwa mahojiano na wanahabari katika studio za
mkundi production zilizopo njiro mkoani Arusha
Kampuni
ya Makundi Production ya jijini Arusha iko katika maandalizi ya kufanya
tamasha kubwa la aina yake litakalo julikana kwa jina la UPENDO WA MAMA
ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba 2014 katika viwanja vya
Sheikh Amri Abeid.
Tamasha
hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili wakubwa kutoka Kenya,
Sara K, na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na Ambwene
Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha
Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila
kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na Kwaya
Mbalimbali.
Lengo
la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA linalengo la kutoa Mitaji kwa zaidi
ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri,
vilevile utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa
upendo waliyonao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na
malezi ya watoto.
Studio
ya Mkundi nakamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa
nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari
kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili
kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA.(Habari picha na Pamela
Mollel wa jamiiblog Arusha)PICHA
HABARI na JIACHIE BLOG