Idadi kamili ya raia wa Afrika Kusini waliofariki ilikuwa 84.
Ndege iliyowabeba manusura wa mkasa huo, kumi na sita kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya, imewasili mjini Pretoria.
Zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea kanisa hilo
la 'All Nations' mjini Lagos, ambalo linaongozwa na mhubiri T.B.
Joshua.
Inaarifiwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.
Mhubiri TB Joshua, amezua wasiwasi baada ya kuzungumzia kuona ndege
iliyokuwa inazunguka juu ya kanisa hilo kabla ya jengo lenyewe
kuporomoka
ZIFUATAZO NI PICHA MBALIMBALI KWA HISANI YA MITANDAO NCHINI NIGERIA
Greda likifanya usaidizi kuondosha kifusi cha jengo la kanisa lilio anguka |
Harufu ikiwa imetanda, vumbi zito likiwa limetawala shughuli ni moja tu ufukuaji. |
Hapa kinachosakwa ni mtu aliye hai au miili zaidi. |
Ni kazi nzito ya kukatisha tamaa. |
Wapi pa kuanzia au tuanzie wapi....?!! |