Sep 23, 2014
Waliopoteza maisha kwenye kanisa lililoanguka la TB Joshua wafikia 115
Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia kuanguka kwa jengo lililopo kwenye kanisa la TB Joshua jijini Lagos, Nigeria, imefikia watu 115, kwa mujibu wa serikali ya Afrika Kusini. Waziri Jeff Radebe wa Afrika Kusini Jumatatu hii ameitaka serikali ya Nigeria inayokosolewa vikali kufanya uchunguzi juu ya
tukio hilo. Tukio hilo lililotokea Sept 12 kwenye eneo la kanisa la mhubiri maarufu, T.B. Joshua, limesababisha vifo vya raia 84 wa Afrika Kusini kutoka kwenye vikundi vya makanisa yaliyomtembelea.
Ajali hiyo imesababisha uhasama wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kubwa kiuchumi barani Afrika.
Waafrika Kusini wamechukizwa na kile wanachokiona kama serikali ya Nigeria inajivuta kufanya uchunguzi juu ya kuanguka kwa jengo hilo na kushindwa kuchukua hatua za haraka kuwaokoa waliokuwa wamenaswa kwenye vifusi.
Joshua na wafuasi wake wanadai kuwa ajali hiyo ni shambulio linalohusishwa na ndege ya ajabu iliyokuwa ikipaa juu ya jengo hilo kabla haijaanguka