Warembo 15 kati ya 30
wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na
mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa
burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo
mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni
washindi watano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji
litakalofanyika jijini Dar es Salaam.
Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.
Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo.
Kila aina ya staili za uchezaji zilioneshwa na warembo hao jukwaani.
Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang,
Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, akiwa na
waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na Mfanyabiashara
Mohamad Bajwa.
Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.
(PICHA NA FATHER KIDEVU BLOG)