Mamia ya
waandamanaj wa Hong Kong wamezingirwa na Askari polisi wanaowataka
kusitisha maandamano na mkusanyiko wao karibu na ofisi za Makao makuu ya
serikali.
Waratibu
wa maandamano hayo wamekaidi amri hiyo na kuwataka watu wengine zaidi
kujitokeza ili kuwaunga mkono katika madai yao ya kuitaka China iwaachie
uhuru wa kumchagua kiongozi wao katika uchaguzi ujao wa mwaka 2017
.
Kiongozi
wa Mamlaka ya Hong Kong C Y Leung amesema serikali yake imesikiliza na
kuzingatia madai ya waandamani lakini inapingana na mpango wao wa
kujitenga.BBC
''Mimi na
serikali yangu tutazingatia sheria za msingi na uamuzi unaostahili wa
NPCSC,tutajaribu juhudi zote kutekeleza uchaguzi wa kiongozi mkuu kwa
kila anayestahili kupiga kura atafanya hivyo mwaka 2017. Serikali
itaanzisha hatua inayofuata ya majadiliano kuboresha katiba hivi hivi
karibuni.
Inasihi
sekta mbalimbali za jamii kushiriki katika majadiliano yenye mantiki kwa
Amani na kwa kufuata sheria, kufikia makubaliano na kukubali tofauti
pamoja na kuruhusu watu milion tano wenye uhalali wa kupiga kura hapa
Hong Kong kumchagua kiongozi mkuu mwaka 2017 mtu mmoja kura moja''
amesema Leung Chung-ying.
'mimi na
serikali yangu tumekuwa wasikivu kwa raia na tumejitolea kudumisha jamii
yote. Wananchi wanatakiwa kutoa wanayoyahitaji kwa Amani, mantiki na
kisheria, na kuheshimu na kuzingatia mitazamo mbalimbali katika jamii.
Serikali
ya SAR ya Hongkong imeazimia kupinga utawala usio wa kisheria wa ofisi
za serikali kuu au makao makuu ya wilaya 'utawala wa seriakli kuu''.
Polisi wanajitambua kukabiliana na hali kwa wakati kwakuzingatia
sheria'' Ameongeza