MADAMUUU! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amecharuka na kudai anachukizwa kwa kiasi kikubwa na wasanii ambao wanapenda kumfanyia majungu kutokana na chuki zao binafsi
.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Madam alisema anajua wapo wengi
wanaomchukia kutokana na sababu zisizo za msingi kwa kudai kuwa anaringa
na vyovyote vile wanavyojadili lakini hajali kwa kuwa hakuna ukweli
wowote.“Watu wenye majungu hawanisumbui kichwa kabisa nabaki nawatazama tu, sababu sina maringo wala majivuno kwa mtu yeyote, sasa cha ajabu wengine wanasema naringa, kwa staili hiyo hatutafika mbali maana wasanii wa nchi za wenzetu wana umoja hawana mambo ya aina hiyo,” alisema Wema.