Muuza sura wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.
Akipiga stori na paparazi wetu, Wastara ambaye aliitendea haki sinema
ya Shaymaa, alisema soko la filamu Bongo bado lipo chini sana kwani
wasanii wengi wanajivunia kwa kujulikana majina bila manufaa ya kazi
zao, tofauti na nchi za nje ambao wasanii wake wanatambulika kwa kazi
zao.“Wasanii wa Kibongo tuna umaarufu maandazi, tunajinadi kwa majina siyo kazi ndiyo maana utakuta mtu ana umaarufu mkubwa lakini kazi zake huzijui, madhumuni yangu ya kuanzisha hii timu ni kwa sababu nataka kupambana niitoe nchi yetu kimasomaso na kukubalika kimataifa,” alisema Wastara