Baadhi
ya wafanyabiashara wa soko la Buzuruga lililoko Wilaya ya ilemela Mkoani
Mwanza,wamelalamikia uongozi wa soko hilo kutokana na hali wizi wa baadhi ya
vitu na bidhaa uliopo soko hapo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara hao
wameeleza kuwa
hali hiyo ya udokozi imekuwa ikiwaweka katika wakati mgumu kutokana na
kupotelewa kwa bidhaa zao nyakati za usiku wanapoziacha na kuelekea majumbani
mwao.
“Tumechoka na huu udokozi wa mali zetu, kila kukicha ni lazima
mali zetu zipotee na tunashindwa kuelewa ni wapi zinapelekwa”alisema Ramadhani
Hussen ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara waliopo katika soko hilo.
Alieleza kwamb, wamekuwa wakiacha biashara zao zikiwa salama na
kamilifu, lakini wanaporudi kesho yake, baadhi yao wanakuta vitu vimepungua na
hawaelewi ni kitugani kinavipunguza.
“Hili soko lina walinzi, lakini kila kukicha tunakuta baadhi ya
vitu havipo, inakuwaje vinapotea wakati watu wa kuangalia usalama wa bidhaa
zetu wapo na tunawalipa”?Alihoji Metusela Obedi ambae nae ni mfanyabishara
sokoni hapo.
Akizungumza kuhusiana na kero hiyo ya wizi ambayo inawakabiri wafanyabiashara
hao, Kaimu Mwenyekiti wa soko hilo Alfan Kazinza, alisema kuwa uongozi wa soko
hilo unafanya kila jitihada ikiwa ni pamoja na
kuwashirikisha wafanyabiashara wa soko hilo kuhakikisha kuwa kero hiyo
inatokomezwa ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha kutoa michango ya fedha itakayosaidia
kupata ulinzi imara katika soko hilo.
Na: Prisca Japhes