Kampuni ya simu inayoongoza barani
Afrika, Asia na Mashariki ya Kati, EtisalatGroup, imeongeza hisa zake katika
kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kufikia asilimia 85. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Zantel jana jijini Dar es Salaam, hatua hiyo ni ongezeko la hisa hizo kwa
asilimia 20 zaidi.
Katika miaka ya hivi karibuni,
Zantel imekuwa ikifanya mapinduzi makubwa katika sekta ya simu za mkononi
Tanzania kwa ubunifu ambao umekuwa ukisaidia kustawisha maisha ya watu. Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na
Z-Kilimo ambayo huwezesha wakulima hata wa vijijini kuweza kupata taarifa
muhimu za jinsi ya kuongeza uzalishaji na hivyo kuendeleza sekta ya kilimo.
Huduma nyingine ni Islamic Portal,
Discover Tanzania (Tourist Portal) na Reverse Ring Back tone (RRBT) ambazo
zinawasaidia watanzania kwa namna mbalimbali.
Pia Zantel ni moja ya kampuni za
simu za mkononi nchini zilizofikia makubaliano na kampuni nyingine za simu
kuwezesha wateja wao kutuma na kupokea pesa miongoni mwao.
Hii ni huduma ya kwanza ya aina hiyo
Afrika ambapo mteja wa kampuni hiyo wa huduma ya EzyPesa anaweza kutuma na
kupokea pesa kwenda mitandao mingine.
Kwa sababu ya juhudi zake katika
kuokoa maisha ya mama na motto, Zantel imeshawahi kupata tuzo inayoheshimika ya
GSMA kwa mradi wa “Mobile Baby”, wakati mkakati wa “Fight Against Malaria”
ulitambulika na Wizara ya Afya.
Habari hii kwa hisani ya Jiachie BLOG