Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya tukio hilo, mengine yameibuka!
Miongoni mwa yaliyoibuka kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili
iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es
Salaam ni madai ya mama Wema, Mariam Sepetu kudaiwa kupewa nafasi ya
kutoa ‘neno la hekima’ lakini akaitumia kumvurumishia mitusi aliyekuwa
shosti wa Wema, Kajala Masanja.
Baada ya sherehe
hiyo, Jumatatu na Jumanne, mitandao mingi ya kijamii ilitumbukiza video
yenye sauti ikimuonesha mama Wema akimrushia matusi Kajala kwa kile
kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kukorofishana kwa mwanaye na Kajala
aliyewahi kumfadhili mahakamani kwa kumlipia faini ya shilingi milioni
13 asiende jela kwa kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa na zuio la kisheria.
Katika kufuatilia sakata hilo,
Amani lilinyetishiwa kwamba Kajala baada ya kushindwa kuvumilia,
ameamua kumshitaki mahakamani mama Wema.
Chanzo chetu kinadai kuwa Kajala alifikia uamuzi huo baada ya
kushauriwa na familia sanjari na wafuasi wake (Timu Kajala) ambapo sasa,
timu hiyo na Timu Wema wameingia vitani tena.
“Kajala ameshawasiliana na wanasheria wawili na kutoa maelezo yake,
wao wanaandaa faili ili mashitaka yafike mahakamani, amekasirika
sana.
“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
Katika sauti, mama Wema anasikika
akitamka matusi (hayaandikiki) huku Wema naye anasikika
akimsihi mama yake asimtaje jina Kajala kwa kuwa kufanya hivyo ni
kumpaisha. Hapa inamaanisha kwamba, Wema alitaka mama yake afunguke
lakini bila kutamka jina la mtu.
Katika
hatua nyingine, mama Wema alisema kauli iliyoashiria kwamba Timu Kajala
ilikuwemo ndani ya bethidei ya mwanaye. “Nasema haya huku najua humu
ndani kuna Timu Kajala, lakini nasema….(matusi mazito)”
Baada ya madai hayo yote, juzi,
Amani lilimsaka Kajala kwa njia ya simu ili kumuuliza ukweli wa madai
hayo. Licha ya kutopokea simu ya mwandishi wetu, alitumiwa ujumbe mfupi
wa maneno ‘SMS’ na kuulizwa kila kitu.
Hata hivyo, badala ya kujibu alikaa kimya, baada ya dakika kama kumi
na tano alimrushia kwa simu mwandishi wetu video hiyo ambayo anadai
kutukanwa na mama Wema bila kusema chochote hali iliyotafsiriwa kuwa
kama alisema; ‘hebu oneni wenyewe jamani, nimemkosea nini mama Wema?’
Katika hatua
nyingine siku hiyo, meneja wa Wema, Martin Kadinda alikuwa na kazi ya
ziada kuhakikisha, mama Wema na mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’
hawakai jirani au meza moja licha ya kwamba watoto wao wamependana.
“Kadinda ana kazi ngumu sana, unajua anatakiwa kuhakikisha kwamba
mama Wema na mama Diamond hawakai meza moja. Sijui anaogopa nini, kwani
hawa si watu ambao watoto wao wana mpango wa kuoana?” alihoji mwalikwa
mmoja.
Katika bethidei hiyo, Wema
alizawadiwa magari mawili, Nissan Murano lenye thamani ya shilingi
milioni 36 alilopewa na Diamond na BMW 545i lenye thamani ya shilingi
milioni 56, inadaiwa alizawadiwa na Kadinda!
Chanzo: Gzeti la Amani/gpl
Chanzo: Gzeti la Amani/gpl