Manchester
United msimu huu imejaribu kujiimarisha katika idara ya ushambuliaji
kwa kufanya usajili wa kuvunja rekodi nchini Uingereza wakiwa na nia ya
kutaka kurejesha makali yao yaliyopotea msimu uliopita lakini uwepo wa
majeruhi takribani tisa ndani ya kikosi cha mashetani wekundu hao
kinaifanya klabu hiyo kuweweseka.
Hivi
karibuni klabu hiyo imetokea kumuamini mlinzi kinda Paddy McNair
aliyekuwa akishirikiana vyema na Muajentina Marcos Rojo katika
kuimalisha ulinzi wa katikati wa klabu hiyo lakini katika kile
kinachoonekana kama kuandamwa na jinamizi la mkosi wa majeruhi kijana huyu naye amelipotiwa kupata maumivu ya misuli daraja la tatu aliyoyapata siku ya Jumapili wakati timu yake ya Manchester United ilipokipiga dhidi ya Everton na kupata ushindi wa magoli 2:1.

Kuumia
kwa McNair kunatimiza idadi ya walinzi watano wa wa klabu ya Manchester
United wanaokaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi ambapo wengine ni
Luke Shaw (kifundo cha mguu), Jonny Evans (kifundo cha mguu), Phil Jones
(misuli) na Chris Smalling (nyama za paja).