Taarifa tulizo zipokea tokea Usiku wa kuamkia leo Tarehe 08-10-2014,
Bado tulikua tukiifanyia kazi kabla yakuiweka kiwanjani, zaashiria
kwamba Msanii Mwanamuziki wa Zamani wa Group Quartier Latin
International BABIA NDONGA SHOKORO kafariki Dunia JIJINI LUANDA (
ANGOLA ),kutokana na MUSHTUKO WA MOYO.
Wengi Wanaambatanisha Kifo chake na kitendo cha
JB MPIANA , FALLY
IPUPA, FELIX WAZEKWA, kumfungulia mashitaka DADA YAKE CHRISTINE maarufu
kwa jina la ” VIEUX KISI NDJORA ” ambae tokea Jana yuku kizimbani kwenye
Jela kuu JIJINI KINSHASA ya MAKALA.
Kwa utafiti wetu, yaonyeshakua, BABIA NDONGA, Tayari alikua na
Matatizo ya Kifamilia katiyake na Mkewe, Usiku wa Kifo chake, Walitokea
kua namabishano makali sana Namkewe, kutokana na hali hiyo, BABIA NDONGA
akatondoka chini, Wakampeleka kwa Haraka kwenye Hospitali Kuu ya PREDA
JIJINI LUANDA ambako umauti ukamkuta.
BABIA NDONGA CHOKORO kajiunga na Group Quartier Latin ya KOFFI
OLOMIDE tokea Mwaka 1993, Album yake ya kwanza aliochangia ni ” MAGIE ”
Iliotolewa Mwaka 1994.
BABIA NDONGA Kajiondoa kwenye Group hilo Mwaka 2001, Kisha akaja tena
kujiunga kwa Mara Nyingine tena na Quartier Latin Mwaka 2003 nakaja
kuamua kujiondoa Moja kwa Moja Mwaka 2011.
Baada yakujiengua kwenye Group Quartier Latin, BABIA NDONGA CHOKORO
kahamia INCHINI ANGOLA JIJINI LUANDA ambako kaweka Maskani yake.
BABIA NDONGA alikua kwenye Matayarisho ya Album yake ” VRAI MOMENT ”
Ukosefu wa Producer wa Uhakika Album hiyo hadi leo haijafaanikiwa
kutolewa.
Salamu zetu za Rambi rambi ziwaendee Familia yake, Tulimpenda sana ila Mwenyezi Mungu kampenda zaidi.
chanzo facebook/cheza kidansi