Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amekuwa Rais wa kwanza aliye mamlakani kufika mbele ya mahakama ya ICC.
Kenyatta
amekanusha tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu anaodaiwa kufanya wakati
wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007/08
Rais Kenyatta alitakiwa kufika kufika mbele ya mahakama hiyo ya ICC ili majaji waweze kuamua ikiwa kesi hiyo itaendelea kusikilizwa au itasitishwa.
Na pia kumuarifu Kenyatta kuhusu malalamiko kutoka kwa viongozi wa mashitaka wa mahakama hiyo kwamba serikali yake imekataa kuwasilisha ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo katika kesi inayomkabili Kenyatta.
Upande wa mashitaka unataka kesi hiyo kuahirishwa hadi serikali ya Kenya itakapowasilisha ushahidi huo.
Nao upande wa utetezi wa Kenyatta unasema Rais huyo hapaswi kufikishwa mbele ya mahakama hiyo kwa sababu upande wa mashitaka umekosa kuthibitisha kesi yake.
chanzo BBC