Mshindi
wa shindano la Serengeti Fiesta Super Nyota Diva 2014 Hellen George
jijini Dar es Salaam, akionyesha makeke yake muda mfupi baada ya
kutangazwa mshindi wa shindano hilo.
Hellen George akifuta machozi muda mfupi baada ya kuibuka mshindi.
...Akiwa
amejiinamia chini baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Dar es Salaam
2014 katika shindano la Serengeti Super Nyota Diva ndani lililokuwa
likifanyika mapema leo ndani ya Ukumbi wa Sun Cirro Sinza jijini Dar es
Salaam.
Mchujo
wa kumpata mshindi wa Serengeti Fiesta Super Nyota Diva kwa wakazi wa
Jiji la Dar es Salaam, umefanyika leo mchana ndani ya Ukumbi wa Suncirro
Shekilango, ambapo tayari vijana mbalimbali wamejitokeza kuchuana na
hatua ya kwanza tayari imemalizika kwa kupata washindi 5, ambao
watachuana ili kuhakikisha anapatikana mshindi mmoja atakayeingia kwenye
fainali za shindano hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Ijumaa hii ndani
ya Ukumbi wa Suncirro kwa kushirikisha wasanii wote waliopatikana
kwenye jumla ya mikoa 14, ambayo imepitiwa na Tamasha la Serengeti
Fiesta 2014.
Mmoja
wa washiriki wa Serengeti Super Nyota Diva, akiwania nafasi ya kuwa
Diva wa Jiji la Dar mapema leo ndani ya Ukumbi wa Suncirro.
Jaji wa mashindano hayo, Elias Barnabas akitafakari jambo wakati mchujo huo ukiendelea.
Mmoja wa washiriki akionyesha uwezo wake katika kuimba.
Majaji
wa shindano hilo kutoka kulia ni mtayarishaji wa nyimbo, Tudi Thomas,
DJ Fetty na Elias Barnabas wakiwajibika kuhakikisha wanampata mshindi
bora wa shindano hilo.
Baadhi ya washiriki wakimshangilia mwenzao wakati akitafuta nafasi ya ushindi jukwaani hapo.
Mmoja wa washiriki hao akikamua kuwania nafasi hiyo.
Washiriki walioingia kwenye tano bora ya Shindano la Serengeti Super Nyota Diva 2014 jijini Dar es Salaam, wakiwa jukwaani.
Mshiriki akiwania nafasi ya kuwa Super Nyota Diva wa mkoa wa Dar es Salaam.
Majaji wa mchujo huo, Barnaba na DJ Fetty wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kutaja washiriki walioingia kwenye tano bora.
Mrembo akiwajibika jukwaani kuwania nafasi ya kuwa Diva wa Dar.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia shindano hilo.
Mshiriki akiwa stejini mbele huku baadhi ya washiriki wenzake wakimshuhudia wakati akiimba.
(HABARI/PICHA: MUSA MATEJA/GPL