Kamati
ya Waamuzi wa mchezo wa kuvuta kamba ikisubiri kumkaribisha Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (hayupo pichani)
aliyetembelea viwanja vya Jamhuri,Morogoro mapema leo kushuhudia michezo
ya kuvuta kamba.
Mwamuzi
wa mchezo wa kamba Bw.Ruvu Kiwanga (kushoto) akisalimiana na Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil alipotembelea
viwanja vya Jamhuri, Morogoro mapema leo.
Baadhi
ya waamuzi wa mchezo wa kamba wakisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil alipotembelea viwanja vya
Jamhuri, Morogoro mapema leo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akikagua timu
ya kamba ya Ikulu alipotembelea viwanja vya Jamhuri, Morogoro mapema
leo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akikagua timu
ya kamba ya Wizara ya Kilimo alipotembelea viwanja vya Jamhuri, Morogoro
mapema leo.
Timu
ya kamba ya Uchukuzi ikivutana na timu ya kamba ya Ujenzi (haipo
pichani) katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika viwanja vya Jamhuri mjini
Morogoro leo. Uchukuzi iliibuka mshindi kwa kuwa na pointi 1-0.
Timu
ya kamba ya Ujenzi ikivutana na timu ya kamba ya Uchukuzi (haipo
pichani) katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika viwanja vya Jamhuri mjini
Morogoro leo.Uchukuzi iliibuka mshindi kwa kuwa na pointi 1-0.
Mashabiki wa mchezo wa kuvuta kamba wakiangalia timu zilizoshiriki kuvuta kamba kwenye uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro leo.
Timu
ya kamba ya RAS Iringa ikivutana na timu ya kamba ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi (haipo pichani) katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika
uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro leo. RAS Iringa iliibuka mshindi kwa
pointi 1-0.
Na Happiness Shayo,Morogoro
Timu
za kamba za Ikulu, Hazina na Mahakama zimeingia hatua ya nusu fainali
kwa kishindo baada ya kuzivuta timu pinzani katika michezo ya SHIMIWI
iliyofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo.
Michezo
hiyo ya kusisimua iliyovuta mashabiki wengi ilianza majira ya saa moja
asubuhi ambapo timu ya kamba ya wanawake ya Ikulu iliivuta timu ya kamba
ya wanawake ya Kilimo na kuibuka mshindi kwa kuvuta mivuto yote miwili.
Mchezo
wa pili ulikuwa kati ya timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Ujenzi
na timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Uchukuzi zilizolazimishana
kutoka droo kwa michezo miwili ya kwanza na hatimaye Uchukuzi kuibuka
mshindi kwa mvuto mmoja baada ya kuvutana kwa mara ya tatu.
Katika
mchezo mwingine timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Mambo ya Ndani
ililazimishana droo na timu ya wanawake ya RAS Iringa na kulazimu
waamuzi kurudia mchezo huo na hatimaye RAS Iringa kuibuka mshindi kwa
kuwa na pointi 1-0.
Mchezo mwingine ulichezwa kati ya timu ya kamba ya wanawake ya TAMISEMI ikiivuta timu ya wanawake ya Mahakama kwa mvuto mmoja.
Kwa
upande wa timu za kamba za wanaume,Ikulu iliibuka mshindi baada ya
kuivuta timu ya NFRA huku Uchukuzi ikiibuka mshindi baada ya kuivuta
timu ya Afya kwa mivuto yote miwili.
Timu
nyingine zilizoingia dimbani kwa upande wa timu za wanaume ni timu ya
kamba ya Mahakama iliyoivuta timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani na kuibuka
na pointi 2 huku timu ya kamba ya Hazina ikiivuta timu ya kamba ya
Maliasili na kuibuka na pointi 2.
Timu
za kamba kwa wanawake na wanaume leo zimetoana katika hatua ya robo
fainali ambapo washindi wataingia nusu fainali itakayochezwa hapo kesho.