Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa
Mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na
vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, juu ya onyesho la Redd's
Miss Tanzania 2014 linalotarajiwa kufanyika Oktoba 11, 2014 katika
Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar.Katikati ni Meneja wa Kinywaji cha
Redd's ambao ni Wadhamini Wakuu wa Mashindano hayo, Victoria Kimaro na
kushoto ni Meneja Maria Stopes Tanzania, Anna Shanalingigwa.
Meneja
wa Kinywaji cha Redd's ambao ni Wadhamini Wakuu wa Mashindano ya Miss
Tanzania, Victoria Kimaro (kushoto) akizungumzia zawadi watakayotoa kwa
Washindi watakaopatikana kwenye Shindano hilo la Redd's Miss Tanzania
2014,ambapo mwaka huu mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro hicho
atajinyakulia kitita cha sh. Mil. 18 taslimu huku washindi wengine
wakiendelea kuondoka na zawadi mbali mbali.Katikati ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Lino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa
Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga na kulia ni Meneja wa Hoteli
ya JB Belmont, Gillian Macheche pamoja na Afisa Habari wa Miss Tanzania
,Hidan Ricco.
Sehemu
ya Wanahabari pamoja na Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro
cha Redd's Miss Tanzania 2014 wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa
Kampuni ya Lino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa
Mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga alipokuwa akizungumza.
Sehemu ya Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014.
Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014 wakipata picha ya pamoja.
(Picha zote na Othman Michuzi)