Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kwaya ya AICT Vijana Makongoro . |
Kwaya ya AICT Vijana Makongoro wakiimba wimbo wa 'Usiichezee amani' |
NA PETER FABIAN, MWANZA.
AIC MAKONGORO VIJANA KWAYA 'Wana Kekundu' wanaotamba hivi sasa na album yao mpya ya “KEUSI” toka Kanisa la African Inland
Charch (AIC) ya Makongoro yamkosha Rais Dkt. Jakaya Kikwete, kwa nyimbo za
Amani na Tukae mezani na kuialika kutumbuiza kwenye maadhimisho ya sherehe za
Uhuru, Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Hatua hiyo ya Rais Dkt. Kikwete kuialika kwaya hiyo
inafuatia hivi karibuni akiwa jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
ya kuzindua miradi ya maendeleo na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara
ya Usagara–Kisesa yenye urefu wa km 16, ilipotoa ujumbe huo wa nyimbo za Amani
na Tukae mezani kumaliza tofauti zetu.
KEKUNDU AIC Vijana Kwaya ilitoa ujumbe huo kwa nyimbo
mbili katika viwanja vya Mabatini Polisi baada ya Rais Dkt Kikwete na ujumbe
wake kuzindua daraja la Mabatini na kisha kwenda kuhutubia wananchi kwenye
viwanja vya Polisi Mabatini na kabla ya viongozi kuanza kuhutubia ilipopata
nafasi ya kutoa ujumbe huo.
Mamia ya wananchi waliofurika wakiwemo viongozi
mbalimbali wa serikali na taasisi, vyama vya siasa na wadau wa maendeleo, kuwa
katika hali ya utulivu kusikiliza ujumbe huo hali iliyoonekana kumgusa kila
mmoja kwa jinsi kwaya hiyo ilivyowasilisha kwa hisia na hata kumkosha Rais Dk
Kikwete na ujumbe wake huku wananchi wakishangilia kwa kupiga makofi.
Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara, Rais
Dkt. Kikwete, alisema nawapongezeni Vijana Kwaya kwa njisi mlivyo tukumbusha watanzania
wote juu ya kuendelea kulinda amani ya taifa hili na kamwe tusiichezee kwani
ikitoweka hatuta ipata tena na wimbo wa tukae mezani kuzungumza na kujadiliana
tofauti zetu na si vinginevyo.
“Asanteni kwa ujumbe wenu mzuri uliojaa maneno ya
kuwakumbusha watanzania juu ya amani, hivyo nawaalika mje kutoa ujumbe huu tena
kwenye maadhimisho ya sherehe za Uhuru Desmba 9 mwaka kwenye uwanja wa Uhuru
jijini Dar es salamu, hakika nimefurahi,”alisisitiza.
PICHA HABARI NA GSENGO BLOG