Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu, wakati
alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwa ajili ya
kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African
Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, iliyofanyika jijini
humo jana mchana.
Maaskofu
wakimwekea mikono ya Baraka Askofu mwenzao, Askofu Mteule wa Kanisa la
African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, wakati
akiwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza jana, Oktoba 19, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristu, waliohudhuria katika Sherehe
za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya
Mwanza, Mchungaji John Bunango, zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza, jana Oktoba 19, 2014.Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya kuwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana Oktoba 19, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu na wanafamilia ya Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya sherehe za kuwekwa wakhfu zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana, machana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu wakati akiondoka kwenye uwanja wa CCM Kirumba, baada ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, jana Oktoba 19, 2014. Picha na OMR.