Mtemvu: Umri wa Binti yangu Miss Tanzania ni Siasa za Wapinzani Wangu Ndani ya CCM
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu amedai
kwamba sakata la binti yake, Sitti Mtemvu, kudaiwa kuchakachua umri
linachochewa na wapinzani wake wa kisiasa ndani ya CCM. Mtemvu alisema
hayo wakati alipokuwa anamtetea binti yake ambaye amedanganya umri ili
aweze kushiriki mashindano ya Miss Tanzania. Binti yake huyo anadaiwa
kuwa kijeba lakini aligushi cheti cha kuzaliwa ili kupunguza umri
uliomwezesha kushiriki mashindano ya u-miss.
Chanzo: Clouds Radio