MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Oct 29, 2014

Mzee Chilo adai ugomvi wa Bongo Movie Unity unatokana na uchu wa madaraka

  Mzee Chilo akizungumza jambo na watoto

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Mzee Chilo amesema ungomvi unaotokea ndani ya Bongo Movie Unity unasababishwa na uchu wa madaraka.
Chilo amesema hakuna chochote kinachogombaniwa zaidi ya madaraka ndani ya tasnia hiyo ambayo amedai imekosa ushirikiano.
“Nimesikia mengi sana kuhusu bongo movie unity, sijui huyu kajiuzulu lakini niseme ukweli tatizo ni uchu wa madaraka,” ameiambia blog hii.
“Kila mtu anamwona mwenzake anakula sana, sasa kwa hali hii hatuwezi fika kokote. Sisi ni wamoja bila kuwa na taasisi za kutuongoza tutaishi vipi? Mimi hawakutaka ushauri wangu kuhusu hili suala ndio maana wala sikuliingilia, wakinihitaji nitawashauri. Kikubwa cha kuwashauri nawataka tushirikiane, tuache tofauti zetu.