Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati alipotembelea ujenzi wa
Daraja la Kigamboni,jijini Dar es Salaam .
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea kadi maalum ya pongezi ya
siku yake ya kuzaliwa Oktoba 07,2014 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau.Rais
Kikwete anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo,akiwa ametimiza miaka 64
toka kuzaliwa kwake.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangaliwa maendeleo ya ujenzi wa Daraja
Kigamboni jijini Dar es Saalam lwakati alipotembelea kuona maendeleo
yake.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alieambatana na Waziri wa Ujenzi,Dkt. John
Magufuli,Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick wakitembelea eneo la Mradi wa Ujenzi
wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam ujenzi huo unafanywa na
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kutembelea eneo hilo.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Serikali,Viongozi wa NSSF pamoja na wakandarasi wanaojenga daraja hilo
mara baada ya kumaliza kutembelea eneo la mradi huo.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na uongozi wa NSSF pamoja na
wajenzi wa Nyumba za Makazi za shirika hilo zinazojengwa Mtoni
Kijichi,jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipatiwa Maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa
nyumba za Makazi zinazojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) katika eneo la Mtoni Kijichi jijini Dar es salaam,wakati
alipotembelea kujionea Maendeleo ya mradi huo
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kwenye jiwe la mradi wa
nyumba za makazi zinazojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF),Mtoni Kijichi,jijini Dar es salaam
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza kwa makini,Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau alipokuwa
akimfafanulia jambo kuhusu mradi huo wa Nyumba.Katikati ni Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.