Mkurugenzi
wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Kipalo Kisamfu(aliyevaa
koti la kaki), na Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Marekani na
mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja kutoka nchini Marekani, Robert Shumake
wakisaini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia
abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara
ya Uchukuzi. Wanaoshuhudia na Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison
Mwakyembe (wan ne kutoka kulia), na wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.
Shaaban Mwinjaka ( wa tatu kutoka kushoto) pamoja na wawakilishi kutoka
kwa Mwanansheria Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Bodi ya TRL.
Balozi
wa heshima wa Tanzania Nchini Marekani na mmiliki wa Kampuni ya M/s
Shumoja , Robert Shumake, akiwaelezea waandishi wa habari(hawapo
pichani), namna treni ya mwendo kasi itakavyotengezwa baada ya utiaji
saini wa Mkataba wa maelewano wa mradi wa treni za kisasa
zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu
kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi
katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi.
Waziri
wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) , akisisitiza jambo wakati
akiongea na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani na na mmiliki
wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake, ofisini kwake kabla ya
kusaini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zijulikanazo kama
Diesel Multiple Unit(DMU) zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar
es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA), leo asubuhi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (mwenye tai
nyekundu), akisisitiza jambo kabla ya utiaji saini Mkataba wa awali wa
mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar
es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi.