Mwendesha mashtaka mkuu kwenye
mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita Fatou Bensouda amesema kuwa
atasitisha uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita ulioendeshwa katika eneo
la Darfur nchini Sudan kutokana na ukosefu wa usaidizi kutoka kwa baraza
la usalama la umoja wa mataifa.
Kwenye taarifa yake kwa baraza
hilo mwendesha mashtaka huyo amesema kuwa wanawake na wasichana
wanaendelea kuathirika zaidi katika jimbo hilo.Amesema kuwa kutokuwepo kwa hatua zozote kutoka kwa baraza la umoja wa mataifa kumechangia kuendelea kwa uhalifu na sasa amelazimika kutumia raslimali za mahakama hiyo kwa masuala mengine.
Mwaka 2009 mahakama ya ICC ilimhusisha rais wa Sudan Omar al-Bashir na uhalifu wa kivita kwenye jimbo la Darfur lakini hadi sasa hajakamatwa wala hata mmoja wa washirika wake.