Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' baada ya kumtembelea leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul
“Diamond” wakati akimuonesha moja ya tuzo kati ya tuzo tano za muziki za
kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne
Desemba 23, 2014. kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na msanii Naseeb Abdul “Diamond” baada
ya kumkaribisha na kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za
kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23,
2014. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko, na kushoto
ni katibu wa Bodi ya filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo.
Rais Dk. Jakaya Kikwete leo amewapongeza
mwanamuziki Diamond Platinumz na mshindi wa shindano la Big Brother
Hotshots Idris Sultan kwa ushindi walioupata hivi karibuni huko nchini
Afrika Kusini.
Rais Kikwete amempongeza Diamond kwa kutwaa
tuzo tatu za muziki za Channel O huku akimpongezza pia Idris kushinda
BBA bila kufanya mambo machafu mjengoni.