Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine tayari kwa tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa huo jijini Mbeya , Mh. Fredrick Sumaye amewaasa watanzania kumcha mungu na kuchagua viongozi waadilifu wenye uzalendo wa nchi, wenye kupenda na kuhurumia wananchi masikini na wenye hofu ya mungu ili kulinda amani ya nchi yetu jambo litakalofanya hata maombi yanayofanyika kuombea taifa la Tanzania yapokelewa na Mungu , Tamasha hilo kesho linaendelea mkoani Iringa ambapo wakazi wa mjini Iringa wanapata nafasi nyingine ya kumcha mungu kwa njia ya uimbaji
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizindua albam ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya yenye inayoitwa Mubhopege Pa Finganilo yenye nyimbo nane kulia ni Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama.
Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu David Mwasota akiiombea albam ya Mubhopege Pa Finganilo ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya huku Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakishiriki katika maombi hayo.
Mwimbaji wa muziki wa injili Upendo Nkone akifanya vitu vyake kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati wa tamasha la Krismas leo.
Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa jukwaani.
Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa akitunzwa na mashabiki wake wakati akiimba jukwaani.
Mwimbaji Emmanuel Mgogo naye amefanya mambo makubwa sana katika tamasha hilo. Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili.
Mwimbaji Joshua Mlelwa akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake na wacheza shoo wake huyu amekuwa pia akifanya maonesho kama haya Ulaya na Marekani ..
Edson Mwasabwite kulia ni Faraja Ntaboba kutoka DRC Congo wakionyesha vitu vikubwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mwimbaji kutoka Kenya Ritha Kisava ambaye ameshiriki Tamasha la Krismas kwa mara ya kwanza akiimba hii ilikuwa kama utabulisho wake kwa mashabiki wa muziki wa Injili nchini Tanzania.
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akiteta jambo na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakati wa tamasha hilo.
PICHA ZOTE NA MICHUZI MATUKIO BLOG