Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amewasiliana na ajenti wa beki wa Real Madrid Sergio Ramos kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kujiunga na kilabu hiyo ya uwanja wa Emirates.
Ramos mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na kilabu hiyo ya Los Blancos kwa takriban muongo mmoja baada ya kuwasili kutoka sevilla kwa kitita cha pauni millioni 20 mwaka 2005.
Hatahivyo ripoti za hivi majuzi zimedai kwamba Ramos huenda akaondoka katika kilabu hiyo ya Santiago Bernabeu baada ya mazungumzo ya kandarasi yake mpya kugonga mwamba.
Na kulingana na mwandishi Esteban Manolete wa AS ,mkufunzi huyo wa The Gunners amewasiliana na wawakilishi wa Ramos ili kuona iwapo anaweza kumvuta mchezaji huyo katika eneo la London kazkazini.
''Wenger amewasiliana na Rene Ramos ajenti na ndugu ya Sergio Ramos'',mwandishi huyo alikimbia kipindi cha La Goleada.
Wenger juma hili alikiri kwamba safu ya ulinzi ya Arsenal haina uongozi baada ya kufungwa bao la dakika za mwisho na liverpool na hivyobasi kupata sare ya 2-2.