Ikiwa zimebaki siku chache kuumaliza mwaka 2014.Muigizaji wa filamu
Shamsa Ford anaetamba mwaka huu kwenye filamu ya CHAUSIKU, amewataka
mashabiki wake na wapenzi wa filamu hapa nchini wamshauri chochote
kuhusiana na kazi zake na maisha yake ya sanaa kwa ujumla.
Shamsa ambae ni mama wa mtoto mmoja, aliweka picha yake nakuandika;
“Ni kitu gani ungetamani kuniambia kabla ya huu mwaka KUISHA”
Jina la Shamsa Ford, lilijitokeza sana mwaka huu kwenye magazeti ya
udaku na mitandaoni baada ya kufananishwa ya yule dada wa kwenye ile
skendo ya muheshimiwa Machemli.
Shamsa Ford amewahi kutamba kwenye filamu kadhaa kama Zawadi ya Birthday, Fisadi wa mapenzi na nyingine nyingi.
Nafasi ni yako mdau, hebu mwambie kitu.