MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 16, 2014

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAFANIKIWA KWA ASILIMIA 98.


Serikali imesema uchaguzi wa  Serikali za Mitaa uliofanyika jana Kote Nchini umefanikiwa kwa Zaidi ya asilimia 98% katika Mikoa yote .

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu mafanikio ya uchaguzi huo.

Akifafanua Mh. Ghasia amesema kwa kiwango kikubwa wananchi walijitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi wao katika ngazi ya Mitaa,Vijiji, na Vitongoji. Akizungumzia mafanikio ya Uchaguzi huo  Mh. Ghasia alitaja Mikoa ambayo uchaguzi umefanyika katika Halmashauri na Kata zote kuwa ni    Arusha,Mbeya,Kagera,Njombe,Singida,Lindi,Ruvuma,Katavi na Geita.

Mikoa Mingine iliyofanya vizuri katika uchaguzi huo ni Iringa,Dodoma,Mtawara ambapo Mh. Ghasia aliwapongeza Viongozi na wataendaji wote wa Mikoa na Halmashauri hizo pamoja na wananchi kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya hadi kufanikisha uchaguzi huo.

Akitoa ufafanuzi Zaidi kuhusu maboresho yaliyofanywa na Serikali katika uchaguzi huo Mh. Ghasia amesema kuwa mojawapo ni kuwepo kwa utaratibu wa kupiga kura kwa kutumia karatasi maalum zilizochapishwa kitu ambacho katika uchaguzi uliopita hakikuwepo.

Akizungumzia Mikoa ambayo baadhi ya Halmashauri zimeahirisha uchaguzi ama Halmashauri yote au sehemu ya Kata zake kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuchelewa kufika kwa vifaa vya kupigia kura Mh.Ghasia aliitaja kuwa ni Kilimanjaro katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Hai,Manyara katika Halmashauri za Hanang na mbulu.

Mikoa Mingine ni Morogoro katika Halmashuri ya Wilaya ya Ulanga na Mvomero,Mkoa wa Shinyanga Halmashauri ya Wilaya ya Msalala,Mkoa wa Simiyu Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Itilima ambapo Mikoa mingine ambayo kasoro ndogondogo zilijitokeza na kupelekea uchaguzi kuahirishwa katika baadhi ya Kata ni    Kigoma,Mwanza,Tabora,Tanga,Mara,Rukwa,Pwani na Dar es salaam.
Akizungumzia Hatua zitakazochukuliwa na Serikali kufuatia dosari zilizojitokeza.