MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 17, 2014

HAPA NA PALE:Chuchu Hans Adaiwa Kumsaliti Ray kwa Mfanyabiashara….Chuchu Afunguka

Inasemekana penzi kati ya waigizaji  Chuchu Hans na Visent Kigosi “Ray” limeingia mtegoni baada ya Chuchu Hans kusemekana kumsaliti mpenzi wake Ray kwa jamaa anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara anayeishi maeneo ya Mbezi Beach Dar.
Chanzo kinasema pamoja na Chuchu kuwa na Ray kwa muda wote, lakini inadaiwa kuwa muda fulani amekuwa akitoka na kwenda Mbezi anapoishi kijana huyo.
Hata hivyo paparazi wetu aliamua kumvutia waya Chuchu na kuzungumza naye ishu hiyo ambapo alidai stori hizo zinasambazwa na watu ambao lengo ni kutaka kumchafua kwa mpenzi wake Ray.
“Watu hawapendi kuniona natoka na Ray na ni hao ndiyo wanaotumia muda mwingi kutaka kutuvuruga. Siwezi kufanya hivi na huyo jamaa sijui wa Mbezi kwanza simfahamu na pili jamii haitanielewa nikifanya hivi,” alisema Chuchu.
Stori na Laurent Samatta

BONGO MOVIE