MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 17, 2014

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Margaret Zziwa aondolewa madarakani

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Margaret Zziwa aondolewa madarakani na wabunge wa Afrika Mashariki na Kumpa saa 24 kukabidhi ofisi hii imekuja baada ya Wabunge wenzake kupiga kura za kutokuwa na imani naye. Bunge la Afrika Mashariki (EALA), limeidhinisha kumuondoa madarakani Spika wa Bunge hilo Mhe. Margaret Zziwa anayetokea Uganda kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka, kutumia vibaya ofisi ya spika pamoja na kutowaheshima wajumbe wa bunge hilo.
Hatua hiyo inafuatia ripoti ya Kamati ya Kanuni na Sheria ya EALA, iliyomtia hatiani Mhe Zziwa na kuridhia kuwajibika mara moja.
Katika kikao hicho kilichokuwa chini ya Mwenyekiti Chris Opoka, ambaye ni Spika wa muda, kura 36 kati ya 39 zilizopigwa na wajumbe wa bunge hilo waliokuwepo walipitisha hoja ya kumvua madaraka Mhe. Zziwa.