Kampuni ya TTCL yatoa msaada Hospitali ya Ocean Road
Mkuu
wa Huduma kwa wateja wa kampuni ya TTCL, Laibu Leonard (wa kwanza
kulia) akimkabidhi baadhi ya misaada Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ocean
Road, Marry Haule (nguo ya bluu) waliyoitoa kwa wagonjwa. Wengine ni
maofisa wa TTCL.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wakishusha bidhaa mbalimbali ambazo wamezitoa kama msaada kwa wagonjwa wa kansa Hospitalini hapo.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ocean Road, Marry Haule (nguo ya bluu) akishukuru TTCL mara baada ya kukabidhiwa msaada huo.