Kundi
zima la Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi, litafanya utambulisho wa
wimbo wao mpya “Sura Surambi” kwa wakazi wa Morogogo Disemba 25 kwenye
maadhimisho ya siku ya Christmas.
Mkurugenzi
wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhani maarufu kama Isha Mashauzi (pichani juu), ameuambia
mtandao huu kuwa onyesho hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Savoy Hotel na
watasindikizwa na mfalme wa kigodoro Msaga sumu.
Isha
amesema “Sura Surambi” ni ngoma yao mpya kabisa iliyoachiwa mwishoni mwa mwezi
uliopita na Morogoro unakuwa ndio mji wa kwanza baada ya Dar es Salaam,
kuonjeshwa ladha ya wimbo huo ambao unafanya vizuri sana kwenye vituo vya
radio.
“Huu
ni utunzi na uimbaji wangu mimi mwenyewe, sina mengi ya kuongea zaidi ya
kuwaahidi wakazi wa Morogoro burudani iliyokwenda shule,” alisema Isha.
Sura
Surambi ni maandalizi ya albam mpya ijayo ya Mashauzi Classic ambapo tayari
nyimbo mbili zimesharekodiwa, hii ikiwa ni pamoja na “Ubaya Haulipizwi”
ulioimbwa na Asia Mzinga, binti wa waimbaji wakongwe wa taarab Abbas Mzinga na Bi
Mwanamtama Amir.