FLORA Mtegoa ambaye ni mama wa marehemu Steven
Kanumba, amesema kuwa Sikukuu ya Krismasi kwake imekuwa mbaya kutokana
na kifo cha mama yake mzazi kilichotokea mwaka huu tarehe na mwezi
aliyofia Kanumba.
Akizungumza na GPL, mama Kanumba alisema kuwa anashindwa kuelewa ni
kwa nini matatizo kwake yanakuja siku ambayo mwanaye Kanumba alifariki
kitu ambacho kinampa wakati mgumu hadi akili yake inashindwa kufanya
kazi.
“Siwezi kusema nina furaha wakati mama yangu hayupo na hiyo ndiyo
inayonipa wakati mgumu wa kutokuwa na furaha kwenye maisha yangu, nina
majonzi ya muda mrefu pengine Kanumba angekuwepo basi ningeweza kula kwa
amani,” alisema.
BONGO MOVIES.COM