Wanasayansi wa Uingereza wanasema
kuwa wanatengeneza dawa kwa watu wanaotafunwa na nyoka wenye sumu kali,
katika nchi za Afrika kusini ya Sahara.
Watafiti katika chuo kikuu
cha matibabu ya magonjwa ya nchi za joto cha Liverpool, wanakusanya
protini kutoka sumu za nyoka wakali kama 400 na wataongeza kemikali ili
dawa iweze kuhimili joto.Wananyonya sumu ya nyoka kama 80 kila wiki.
Inakisiwa kuwa watu 30,000 wanakufa kila mwaka kwa sababu ya kutafunwa na nyoka.