lipuaji wa kujitolea muhanga amejilipua katika soko moja katika mji wa kazkazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.Baadhi ya ripoti zinasema kuwa mlipuaji huyo ni msichana wa miaka kumi.
Duru kutoka hospitali zimeambia BBC kwamba takriban watu 15 wameuawa.
Hakuna mtu aliyekiri kutekeleza shambulizi hilo kufikia sasa.
Hatahivyo
watu wanalishuku kundi la Boko Haram kutokana na misururu yake ya
mashambulizi katika mji huo na maeneo mengine ya Nigeria Kazkazini.
Takriban
watu elfu ishirini wamelazimika kutoroka na inahofiwa kuwa mamia
waliuawa wakati Boko Haram lilipochukua udhibiti wa mji wa Baga na
viungani mwake wiki iliopita.
chanzo BBC