Mrembo na mwanamitindo ambae pia ni mwigizaji wa filamu na
ujasiriamali, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amemrushia maneno makali aliyewahi
kuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa hana akili
timamu kufuatia maneno aliyotoa kuwa enzi za uhusiano wao, eti mwanadada
huyo alikuwa akichenga kumzalia mtoto.
Hivi karibuni akizungumza na Global TV online,
Diamond alifunguka: “Jokate na Wema (Sepetu) nilitamani sana wanizalie
lakini walikuwa wakichengachenga, mambo mengine ujue si ya kuzungumza
lakini inauma.”
Kufuatia tuhuma hizo nzito huku kukiwa na madai pia, kwamba Jokate
aliwahi kupigwa mimba ‘akaipanchi’, mwanadada huyo alipotafutwa na
mwandishi wetu kujibu ‘shitaka’ linalomkabili alianza kwa kumshangaa
Diamond.
Jokate alisema anamshangaa Diamond kuyazungumza maneno hayo hadharani na
inaonesha asivyokuwa na akili timamu au ambayo haijakomaa.
“Diamond atuache, kila siku anatuzungumzia, hana akili timamu.
“Inadhihirisha kweli hana akili kwa kuwa mtu mwenye akili zake timamu
hawezi kwenda kwenye chombo cha habari na kueleza hayo aliyoyasema,”
alisema Jokate akionesha kukasirishwa na maneno ya Diamond.
BONGO MOVIES.COM