Mwigizaji wa filamu hapa bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa, licha
ya ujauzito wake kuwa mkubwa, mume wake Sunday Demonte hana taarifa
yoyote juu ya kitumbo hicho
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na mwigizaji huyo, amethibitisha kwamba
ni kweli ujauzito wa Aunty sio wa mume wake ni wa dansa wa Naseeb Abdul
‘Diamond Platnumz’ aitwaye Moses Iyobo.
“Ni kweli ujauzito wa Aunty ni wa mpenzi wake na si mumewe. Unajua
anatoka na Iyobo na wawili hao bado wanaonekana pamoja, hafanyi tena
safari za Dubai ambako ndiko mumewe aliko,” kilisema chanzo hicho.
Aidha Aunty Ezekiel alidai kuwa yeye na mume wake huyo hawajaachana
na hajapewa talaka kama watu wanavyodai lakini hajui kwamba ni mama
mtarajiwa na hata akijua hawezi kumuacha.
“Kiukweli mume wangu hajui kuwa nina ujauzito na hata akijua wala
hawezi kuniacha, ananipenda sana. Sijaachana naye na wala sijapewa
talaka, hayo yanayosemwa ni umbeya tu,” alidai Aunt.
Ngoja tusubiri kama bado kuna ndoa hapa.
BONGO MOVIE.COM