Meli kubwa zaidi duniani imetia
nanga nchini Uingereza kwa mara ya kwanza wakati huu ikiendelea na
safari yake duniani, je Meli hii ina nguvu kiasi gani na ukubwa gani?
Meli
iitwayo the Globe ina urefu wa mita 400 ikifananishwa na ukubwa wa
mabwawa manane yanayotumika katika michuano ya Olimpiki ina upana wa
mita 56.8 na upana wa mita 73 kwenda juu, ina uwezo wa kubeba mzigo wa
tani 186,000.Shuhuda wa Meli hiyo anasema ''ukiitazama meli hiyo utajihisi mbilikimo ni Meli kubwa mno''.
Safari ya Meli hiyo ilianzia mjini Qingdao nchini China tarehe 3 mwezi Desemba mwaka jana na inatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 25 Februari.
Hii ni meli ya kwanza kubwa zaidi kati ya meli kubwa tano zenye umbile kama Globe kutengenezwa Korea kusini, Meli zote zinatarajiwa kutolewa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.