Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistani, Chaudhry Nisar
Bunge nchini Pakistani limepitisha
maamuzi ya kuundwa kwa mahakama za kijeshi kwa ajili ya kuwashtaki
Wanamgambo wanaoshutumiwa kutekeleza vitendo vya kigaidi.
Mabadiliko
haya ya Katiba ya Pakistani ni sehemu ya mfululizo wa hatua
zinazochukuliwa kupambana na wimbi la mashambulizi yanayotekelezwa na
wanamgambo wa Taliban ikiwemo mauaji dhidi ya watoto wa shule mwezi
uliopita.Vyama vingi vimebariki hatua hiyo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa mahakama za kiraia zimeonyesha kushindwa kuwafikisha wanamgambo kwenye mikono ya kisheria.
Waziri wa mambo ya ndani,Chaudhry Nisar Ali Khan amesema mahakama za kijeshi zitakuwa na mamlaka kwa kiasi fulani.