MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 12, 2015

RAIS DK KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 51 YA MAPINDUZI ZANZIBAR LEO

unnamed5Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh.Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mh. Dr. Ali Mohammed Shein.
unnamed6
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh.Dr. Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mh. Dr. Ali Mohammed Shein.

unnamed1h
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia Mkono wananchi wakati alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika leo.
unnamed2h
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama leo wakati wa Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar akifuatana na Paredi Kamanda Luteni kanali Mohamed Khamis Adam katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
unnamed1
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu Mh Benjamin Mkapa wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani, Katikati ni mama Fatma Karume na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim.
unnamed2
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh.Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katikati ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar Mh. Shamsi Vuai Nahodha.
unnamed3
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh.Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassani Mwinyi.
unnamed4
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh.Dr. Jakaya Kikwete akizungumza na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa maadhimisho hayo mjini Zanzibar leo.
unnamed4h
Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za kilele cha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika kilele hicho Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
unnamed7h
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika leo katikauwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
(Picha na Freddy Maro wa Ikulu).