Katibu
Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC), Chande Omar (kulia)
akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) kabla ya kuanza kwa sherehe za
uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani iliyopo Kusini Pemba. Katikati ni Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph na kushoto ni
Mke wa Mratibu Mkazi wa UN Tanzania, Bi. Fainula Kurji-Rodriguez.
Meneja
wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Mkoani Kusini Pemba, Bw. Ali
Abbas akisoma risala ya kituo chake mbele ya mgeni rasmi Waziri wa
Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto visiwani
Zanzibar, Mh. Zainabu Omari Mohammed (hayupo pichani) wakati wa sherehe
za uzinduzi wa kituo hicho cha redio.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo visiwani
Zanzibar, Juma Yakufi akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri mwenye dhamani
ya wizara hiyo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani jimbo
la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba uliofanyika mwishoni mwa wiki
visiwani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba, Hemedi Selemani akitoa neno la
shukrani wakazi wa mkoani jimbo la Mkanyageni pamoja na wageni waalikwa
kwenye sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba
uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza kwenye uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba
uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akimkabidhi cheti Meneja wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba, Bw. Ali
Abbas wakati wa sherehe za uzinduzi wa Redio jamii hiyo.
Meza kuu.
Mkuu
wa Mkoa wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba, Bi. Mwanajuma
Abdallah akizungumza machache na wakazi wa mkoani na kuwaasa kukitumia
chombo hicho vyema katika kujiletea maendeleo na kupashana habari kabla
ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua rasmi kituo hicho cha Redio Jamii.
Waziri
wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab
Omar Mohammed akisoma hotuba yake kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo
cha redio ya jamii jimbo la Mkanyageni, Mkoani Kusini Pemba.
Mabinti
wa visiwani Pemba wakisoma utenzi wa kulishukuru shirika la UNESCO na
ZBC kwa kuanzisha kituo hicho cha Redio jamii jimbo la Mkanyageni mkoani
Kusini Pemba.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wakazi wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini
Pemba wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi kwenye sherehe za
ufunguzi wa kituo hicho cha Redio Jamii.
Pichani
juu na chini ni Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake
na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akikabidhi vyeti kwa baadhi ya
wafanyakazi wa Redio Jamii Mkoani ya jimbo la Mkanyageni mkoani Kusini
Pemba. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja
wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo visiwani Zanzibar, Juma Yakufi.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na
watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi
wa kituo cha Redio Jamii Mkoani iliyopo Kusini Pemba. Wanaoshuhudia
tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba,
Bi. Mwanajuma Abdallah (mwenye mtandio wa bluu), Mkuu wa Wilaya ya
Mkoani Kusini Pemba, Hemedi Selemani pamoja na Mratibu Mkazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Sasa kimezinduliwa rasmi....!
Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na
watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akitia saini kitabu cha wageni cha
kituo cha Redio Jamii Mkoani Kusini Pemba kabla ya kukagua vifaa na
studio ya kituo hicho.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na
watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akizungumza Live na wananchi wa jimbo
la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba mara baada ya kuzindua kituo cha Redio
Jamii Mkoani ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za Mapinduzi mwishoni
mwa wiki kisiwani Pemba. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na washika dau kutoka UNESCO.
Mtangazaji
wa kituo cha Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba, Bw. Seif Mohammed
akiwa kwenye mahojiano na Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa
jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed yaliyorushwa
Live na kituo hicho mara baada ya kuzinduliwa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na
watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed katika picha ya pamoja na wafanyakazi
wa Redio Jamii Mkoani, Wajumbe wa Bodi ya Redio Jamii Mkoani, wafadhili
pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na
watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed katika picha ya pamoja na wajumbe wa
bodi ya Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba.
Mshauri
na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akiwa kwenye picha na wanafunzi
wake wa vituo vya redio jamii ya Mkoani na Micheweni mara baada ya
sherehe za uzinduzi.
Kikundi
cha Ngoma ya Msembwe cha kisiwani Pemba kikitoa burudani kwenye
uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani uliofanyika mwishoni mwa juma Kusini
Pemba.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye
koti la suti) akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili
kuhuduria sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni,
Kusini Pemba na kupokelewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na
Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
Bw. Al Amin Yusuph (kulia) aliyeambatana na Mshauri na Mkufunzi kutoka
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi.
Rose Haji Mwalimu (aliyeongoza mbele).
Na Mwandishi wetu, Pemba
SERIKALI
ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba itaendelea kuruhusu kuanzishwa kwa
Redio za jamii kutokana na umuhimu wake katika kuhimiza maendeleo na
kutumika kama daraja kati ya wananchi na serikali yao.
Hayo
yalisemwa na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na
watoto, Zainab Omar Mohammed wakati akizundua kituo cha redio ya jamii
jimbo la Mkanyageni, Mkoani Pemba.
Shughuli
hiyo ambayo ilifanyika kama sehemu ya shamra shamra za sherehe za
mapinduzi kutimiza miaka 51 zilihudhuriwa pia na wafadhili wa mradi huo
ambao ni Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO).
Waziri
huyo alisema kwamba uzinduzi wa kituo cha redio ya jamii katika jimbo
la Mkanyageni Mkoani Pemba ni moja ya azma ya serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kuwapa haki wananchi wake ya kupata habari ikiwa ni sehemu
muhimu sana ya maisha ya wanadamu.
Munekano wa sehemu ya jengo la Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba kabla ya kuzinduliwa rasmi.
Alisema
habari ni kitu muhimu sana katika maisha ya sasa na wakati taifa
likiadhimisha miaka 51 ya mapinduzi yaliyolenga kubadili maisha ya
wazanzibari uwapo wa redio za jamii ni kitu ambacho kitasukuma mbele
zaidi madhumuni ya mapinduzi , kumkomboa mzanzibari kiuchumi na
kifikira.
“Redio
hizi Jamii, zimewekwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
madhumuni ya kuwapa fursa wananchi kupata habari,kupata burudani, kupata
elimu, lakini pia kutoa fursa ya kutoa mawazo yao kupitia redio hizi
ili serikali ipate kujua zaidi nini hasa changamoto za wananchi na iweze
kuzifanyia kazi kwa urahisi zaidi” alisema Waziri Zainab.
Pamoja
na kuushukuru Umoja wa mataifa kwa kusaidia redio za jamii aliutaka
Umoja huo uendelee kuimarisha uwezo wa redio hizo ili wananchi wazitumie
kupata maendeleo.
Naye
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
amesema Umoja wa mataifa unajisikia fahari kuwezesha asilimia 60 ya
wazanzibari kusikiliza redio za jamii na kuzitumia katika maendeleo yao.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
aliyeambatana na mkewe akisalimiana na Ofisa mdhani kutoka Wizara ya
Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya
usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed mara baada ya kuwasili eneo
la tukio.
Alisema
umoja huo utaendelea na ushirikiano wake na serikali ya Mapinduzi
Zanzibar ya kuweka mazingira ya upatikanaji wa habari kuwa bora zaidi,
ushirikiano ambao waliuanza mwaka 2008 wakati wa kutengeneza sera ya
utangazaji. Alisema ni sera hiyo iliyowezesha kuwepo kwa redio za jamii
na utangazaji wa umma.
Alisema
Redio za jamii ni msaada mkubwa katika kutoa elimu kwa jamii
inayozunguka kituo hicho na kusema kwamba ni imani yake kituo cha Mkoani
kitafanya kazi iliyokusudiwa kwa kuhamasisha mawazo chanya ya maendeleo
na kuleta ushirikiano na amani inayotakiwa katika jamii.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa
la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph wakipitia
ratiba kabla ya kuanza rasmi sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani
uliofanyika Kusini Pemba.
Amesema
Umoja wa Mataifa umewezesha kituo hicho vifaa vya utangazaji na
kutengeneza uwezo wa wafanyakazi wa chombo hicho. Amesema kupitia mradi
wa uwezeshaji demokrasia (EDP) unaoendeshwa kwa pamoja na UNESCO na
UNDP chini ya makubaliano ya msaada kwa serikali ya Tanzania na Umoja wa
Mataifa (UNDAP) , Umoja wa Mataifa umetoa mtambo wa kurushia matangazo
wenye nguvu za Watts 600 unaoweza kusambaza matangazo yake eneo lote la
Kusini pemba.
Pamoja na mtambo huo na vifaa vingine vya studio vilitolewa na
kumefanyika ufundishaji wa watangazaji namna bora ya mawasiliano na
menejimenti ya habari na utawala. Mratibu huyo aliitaka serikali na
taasisi zake kukitumia vyema kituo hicho katika kuhakikisha kwamba
maendeleo yaliyokusudiwa kwa jamii yanapatikana kupitia vipindi
mbalimbali vya kuelimishana.
Mke
wa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bi. Fainula
Kurji-Rodriguez (kushoto) na Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji
Mwalimu wakifurahia burudani ya Ngoma ya Msembwe ya Kusini Pemba
ilipokuwa ikisherehesha kabla ya kuwasili wa mgeni rasmi katika uzinduzi
huo.
Pia
aliwataka waendeshaji wa kituo hicho kuwa makini na kuwajibika kwa
umma, kauli ambayo awali pia ilielezwa na Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya
habari Utamaduni , Utalii na Michezo Juma Yakufi aliyetaka sheria na
taratibu za mawasiliano kuzingatiwa.
Alitaka
vipindi vitakavyotengenezwa kuzingatia utu, silka na utamaduni wa
Mzanzibari na redio hiyo kuendeshwa kwa mujibu wa masharti ya redio
jamii kwa kuhakikisha hawaingiliwi na taasisi yoyote na kuendeshwa kwa
manufaa ya jamii na sio manufaa ya mtu mmoja mmoja.
Naye
Mwa redio hiyo Ali Abbas pamoja na kushukuru kusaidia kuanzishwa kwa
redio hiyo aliitaka jamii kuitumia vyema nafasi waliyopewa kuendeleza
mbele maendeleo yao na kutumia upashanaji habari kutanzua changamoto za
maendeleo.
Mshauri
na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akijumuika kutoa burudani na
kikundi cha Ngoma ya Msembwe kutoka Kusini Pemba.
NA JIACHIE BLOG