Shirika la riadha nchini AK limetoa orodha ya sheria za kukabiliana na wanaraidha wanaoutumia dawa za kusisimua misuli huku kukiwa na ongezeko la ripoti kuhusu wanariadha wa Kenya ambao wamefeli ukaguzi wa dawa hizo.
Sheria hizo zimetolewa siku tatu kabla ya mshindi mara tatu wa mashindano ya Boston Marathon Rita Cheptoo kufika mbele ya tume ya kukabiliana na dawa hizo katika shirika la riadha la Kenya AK ambapo kesi yake itasikizwa.
Cheptoo wa Kenya alifanikiwa kulitetea taji lake la Boston Marathon alipoweka rekodi ya masaa 2 dakika 18 na sekunde 57.
Mwanariadha huyo ni mshindi wa 73 wa mashindano ya Boston.
Lakini Cheptoo alifeli ukaguzi wa dawa za kusisimua misuli mnamo mwezi Septemba 2014.
Cheptooo ni miongoni mwa wanariadha kadhaa wa Kenya wanaochunguzwa kwa kutumia dawa za kusisimua misuli.