Wanyama walipatiwa tuzo mjini Bangalore na Mwanasiasa Vatal Nagaraj, Kiongozi wa chama kimoja mjini humo. Mtandao wa NDTV umeripoti.
Mwanasiasa huyo amesema ameamua kutoa tuzo kwa wanyama kama Punda, Mbwa, Swala,na Ng'ombe kwa kuwa waaminifu kuliko binadamu, wanafanya kazi kwa bidii,wana adabu na heshima.
Nagaraj aliwapamba wanyama hao kwa maua wakati wa tukio la kuwatunuku.
Wakiwa wamevalia shanga zenye rangi za kupendeza, Punda waliwafurahisha watazamaji waliokusanyika katika sherehe hiyo.
Mwanasiasa huyo amesema Punda hutumika kwa kiasi kikubwa kuchapa kazi nchini India, mara nyingi hawatiliwi maanani.
Hakuna vigezo vigezo vya maombi, wala hakukuwa na majaji wa kuwachagua washiriki.yalikuwa mashindano ya kipekee ya tuzo ulimwenguni, Nagaraj alisema kabla ya shamrashamra hizo.