Eneo ambalo washukiwa wa Charlie Hebdo wamezingirwa nchini Ufaransa
Milio ya risasi imesikika na kuna ripoti ya kukamatwa kwa mateka mmoja huku maafisa wa polisi wa Ufaransa wakiwazingira washukiwa waliohusika na mauaji ya Charlie Hebdo.
Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa katika eneo la Dammartin-en-Goele yapata kilomita 35 kutoka Paris,lakini maafisa wamekana ripoti ya mauaji yoyote.
Majadiliano ya polisi yanaendelea ripoti zimesema.
Mpango huo unajiri karibia masaa 48 baada ya shambulizi hilo katika afisi za gazeti hilo ambapo watu 12 waliuawa kwa kupigwa risasi.
Washukiwa hao wanaodaiwa kujihami vilivyo baadaye waliutoroka mji wa Paris kupitia gari moja.
Msafara wa mgarai ya polisi umeonekana ukielekea katika eneo la Dammartin-en-Goele.