Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea
malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za
filamu uliotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment.
Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei
iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na
itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika
tasnia ya filamu.
Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza
kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka
utakapopatikana katika kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya Habari,
Vijana,Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na
Biashara.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.